Mastaa

MC Pilipili Kuzikwa Leo

DODOMA: MSANII wa vichekesho Emmanuel Mathias, maarufu kama Mc Pilipili, ambaye amefariki dunia Novemba 16, 2025 , anatarajiwa kuagwa na kuzikwa leo nyumbani Swaswa, mkoani Dodoma, Ibada Kuu kufanyika Chinangali

Kwa mujibu wa taarifa za familia, mwili wa marehemu utatolewa nyumbani kwao Swaswa, kisha kupelekwa Viwanja vya Chinangali ambapo ibada kuu na shughuli ya kuaga mwili itafanyika.

Wananchi, ndugu, jamaa na marafiki watapata nafasi ya kutoa heshima za mwisho.

Baada ya ibada na kuagwa, mwili wa MC Pilipili utapelekwa kwenda kupumzishwa katika nyumba yake ya milele kwenye makaburi ya Ipagala Kilimo Kwanza, jijini Dodoma.

Familia imeendelea kuwaomba watanzania kuendeleza upendo na maombi wakati huu wa maombolezo ya kumpoteza mmoja wa vijana waliokuwa wakileta furaha na burudani kwa jamii

Related Articles

Back to top button