Nyumbani

Master Rim FC kuunga mkono utalii

KATIKA kuunga mkono jitihada za serikali kutangaza utalii, timu ya soka ya Master Rim FC imejipanga kutangaza utalii nchini kupitia jezi zao, mmiliki wa timu hiyo Kassim Ahmed ameileza HabariLEO.

Master Rim FC ni timu ambayo kwa sasa inakamilisha hatua za mwisho za usajili kushiriki ligi daraja la tatu za mikoa, iliwahi pia kucheza mashindano ya Ndondo Cup msimu uliopita pamoja na mashindano ya Ramadhan Cup.

Akizungumzia mipango ya timu hiyo, Kassim Ahmed amesema kwanza wamepanga kuanza kwa kuandika maneno yanayosomeka Serengeti Nationl Park mbele ya jezi zao, kisha baadaye watakuja na Royal Tour.

“Tumejipanga sana kwanza kuinua vipaji na kutangaza utalii kwa nchi nchi yetu kwa kuweka maneno ya Serengeti National Park na Royal Tour kwenye jezi zetu,” amesema Ahmed.

Pia amezungumzia mipango ya kucheza Ligi Kuu ambapo amesema kwasasa wanakamilisha usajili kushiriki ligi daraja la tatu na baada ya hapo wamejiandaa kwa kuzingatia kuwa ⁠bajeti yao inatosha kucheza mashindano makubwa.

“Kabisa tena na pia tumeshaongea na wadhamini mbalimbali kwa mfano kama kampuni za simu kama mbili zote hizo zipo tayari kutuunga mkono,” amesema Ahmed.

Related Articles

Back to top button