Michezo Mingine

Majaliwa mgeni rasmi TASWA bonanza

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika bonanza maalumu la waandishi na wafanyakazi wa vyombo vya habari ‘TASWA Media Day Bonanza 2024’ Februari 10.

Taarifa ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo(TASWA) imesema wakati wa bonanza litakalofanyika Dar es Salaam pia kutafanyika uzinduzi wa Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2024 zinazotolewa na TASWA.

TASWA imesema bonanza hilo litatumika kuzindua kama zake mbalimbali za kiutendaji ambazo ni mafunzo na maadili, fedha na mipango, Ukaguzi wa hesabu, Katiba, tuzo za wanamichezo bora na kamati ya wanawake na michezo.

Lengo la bonanza hilo ni kuwakutanisha waandishi na wafanyakazi wa kada nyingine katika vyombo vya habari ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.

Michezo ya aina mbalimbali itafanyika wakati wa bonanza hilo linalotarajiwa kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 2000 ikiwemo mpira wa miguu, kikapu, wavu, pete ikichezwa ufukwe wa klabu ya Msasani.

Related Articles

Back to top button