Leonardo: Mwanaume unapaswa kumuamini mpenzi wako

DAR ES SALAAM: MKALI wa vichekesho, Leonard Butindi, amesema kuwa kuwa na mpenzi mzuri wakati mwingine kunaweza kumfanya mwanaume kuwa na wasiwasi, hasa kutokana na mazingira ya jamii na namna watu wanavyomzunguka.
Leonard amesema mwanamke wake ni mtu anayejitambua na anayejiheshimu katika kila jambo, jambo linalompa amani lakini pia kumfanya awe makini zaidi.
“Mwanamke wangu anajielewa na anajiheshimu kwa kila kitu, ikiwemo mavazi yake, maongezi yake, hata uigizaji wake,” amesema Leonard.
Ameeleza kuwa tatizo si mwanamke kuwa mitandaoni au kutokuwa maarufu, bali ni namna mwanaume mwenyewe anavyolichukulia suala hilo na jinsi anavyojenga imani kwenye uhusiano.
“Kiukweli shida si mwanamke kuwa mitandaoni au kutojulikana. Mwanamke akiwa mzuri, mwanaume unaweza kuwa na hofu naye. Lakini mwanaume unapaswa kumpa mpenzi wako ndoto zako na kumuamini,” amesema.
Aidha, msanii huyo amesema licha ya kufanya kazi pamoja na mpenzi wake, hamthibiti wala kumbana, bali anaishi naye kwa kuaminiana na kuelewana.
“Binafsi nafanya naye kazi, simthibiti, bali najua ni aina gani ya mwanamke niliye naye, kwa sababu mjini kuna mambo mengi na watu ni wengi,” ameongeza.




