Mastaa

Lamata: Nilihusika kuwakutanisha Kajala na Harmonize

MTAYARISHAJI wa filamu Leah Mwendamseke ‘Lamata’ amefunguka kuhusu sababu ya kuwakutanisha msanii wa filamu Frida Kajala na msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’.

Wawili hao, ambao hapo awali walikuwa wapenzi hadi kufikia hatua ya kuvalishana pete, walijikuta wakiachana na kutupiana maneno mitandaoni. Hata hivyo, walifanikiwa kukutana tena uso kwa uso katika mechi za Samia Cup zilizotamatika hapo jana Machi 25.

Lamata amesema, “Kweli nilikuwa kiunganishi cha wawili hao kwa kuwa wote ni watu wangu wa karibu, hivyo wakawa pamoja. Yaliyoendelea baada ya hapo ni yao wenyewe.”

Mbali na hilo, Lamata ameongelea pia maendeleo ya timu yake, Lamata Village SC, akieleza safari yake tangu mwanzo wa mawazo yake hadi leo, ambapo timu hiyo imepata Shilingi Milioni 5 kutoka Selcom.

“Nilianzisha timu ya Lamata Village kama utani, lakini naona wakiendelea kufanya vizuri hadi kufikia hatua ya kushinda kiasi cha sh milioni 5, sio jambo dogo,” amesema Lamata.

Related Articles

Back to top button