EPLKwingineko
Kurasa za mwisho za Degea Manchester United

MLINDA LANGO wa Manchester United David Degea anatarajiwa kuondoka ndani ya timu hiyo mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa mwezi Juni 2023.
Taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya zimeeleza kuwa Degea ameshindwa kukubaliana na Manchester United ili asaini mkataba mpya ambapo United wanamtaka kipa huyo kupunguza mshahara lakini wamegonga mwamba.
Degea mwenye miaka 32 ameitumika Manchester United kwa miaka 12 tangu alipojiunga nao mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid ya Hispania.
David Degea ameichezea miamba hiyo ya jiji la Manchester United michezo 545 na kuondoka na hati safi ( Clean sheet) 190.
Klabu mbalimbali kutoka mataifa ya Uarabuni zinahusishwa kuitaka huduma ya Degea atakapoamua kuachana na Manchester United.




