‘Kombolela’ yaibuka Tamthilia Bora Tamasha la Ziff 2025

ZANZIBAR: TAMTHILIA pendwa nchini ‘KOMBOLELA’ inayorushwa na Azam TV imeibuka kidedea katika Tamasha la 28 la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) mwaka 2025, ikinyakua tuzo ya Tamthilia Bora ya Tanzania.
Hii ni heshima kubwa kwa Mustapha Machupa ambaye ndiye muongozaji wa tamthilia hiyo iliyovutia wengi katika tamasha hilo.
Kombolela imethibitisha kuwa ni miongoni mwa tamthilia bora kabisa zinazopatikana nchini Tanzania kwa muigizaji wake Shamira Ndwangila kunyakua tuzo ya muigizaji bora wa kike katika tamthilia nchini Tanzania.
Ushindi huu unaongeza chachu katika tasnia ya filamu na tamthilia Tanzania, ukiashiria ukuaji na ubora wa kazi zinazofanywa na wasanii.
Mafanikio haya ya Kombolela yanaendana na mafanikio mengine ya Tanzania katika ZIFF 2025 ambapo Kojack Chillo (Jacob’s Daughters) amenyakua tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume katika Tamthilia (Tanzania).
Muigizaji Wisher Nakamba (Niko Sawa) alikuwa Muigizaji Bora wa Kike (Tanzania) na Hemedy Suleiman (Niko Sawa) alikuwa Muigizaji Bora wa Kiume (Tanzania).