EPL
Kocha Brighton kuikosa United leo

KOCHA wa Brighton, Roberto De Zerbi ameripotiwa anaumwa na huenda asiwe sehemu ya mhezo wa leo dhidi ya Manchester United.
Beki Joel Veltman alichechemea kipindi cha pili dhidi ya Wolves, huku Evan Ferguson pia kukiwa na shaka kama atatumika katika mchezo.
Mshambulizi wa Manchester United, Alejandro Garnacho amerejea mazoezini lakini mchezo huu unakuja mapema sana kwake kuweza kurejea kutokana na jeraha.
Scott McTominay na Raphael Varane pia wanasalia nje ya uwanja na Lisandro Martinez yuko nje kwa msimu huu.