Featured

IFAB yatangaza kiama kwa Magolikipa

ZURICH: Bodi ya Kimataifa inayosimamia mpira wa miguu (IFAB) imepitisha kanuni mpya ambayo inatazamiwa kudhibiti vitendo vya upotezaji wa muda kwa walinda lango kwa kutoa pigo la Kona kuelekea kwa timu ya golikipa ambaye atashikilia mpira kwa Zaidi ya sekunde 8.

Kanuni hiyo imepitishwa kwa kura zote katika kikao cha IFAB kilichofanyika leo katika makao makuu ya shirikisho la soka duniani FIFA Mjini Zurich nchini Switzeland na inatarajiwa kuanza kutumika msimu ujao kwenye ligi na mashindano ya mashirikisho yaliyo chini ya bodi hiyo.

Huenda golikipa wa Wolves ya Ligi kuu ya England akawa mhanga mkubwa wa kanuni hii kwani tangu ajiunge na Wolves amekuwa na kadi nyingi za njano ambazo nyingi zinatokana na tabia yake ya kupoteza muda hasa timu yake hiyo inapokuwa na nafasi ya ushindi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button