Hazard ataka waamuzi kulinda wachezaji
						WINGA wa Ubelgiji Eden Hazard ametaka waamuzi katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea Qatar kulinda wachezaji dhidi ya kufanyiwa madhambi.
Mbelgiji huyo alikuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Doha, Qatar leo kuelekea mchezo wa nchi yake dhidi ya Morocco kundi F utakaopigwa Novemba 27 katika uwanja wa Al Thumama.
Hazard ni wa pili kwa kufanyiwa madhambi mengi zaidi nyuma ya Neymar baada ya raundi ya kwanza katika michuano hiyo.
“Wachezaji wengi wakiwa na mpira kama mimi, kama Neymar, kama Vinicius Junior, tunaweza kufanyiwa madhambi. Tunapaswa kukabiliana hii hali.Ni sehemu ya mchezo,” amesema Hazard.

Neymar ambaye alifanyiwa madhambi mara 9 katika mchezo uliopita wa Brazil dhidi ya Serbia atakosa michezo miwili ya mwisho ya timu yake kundi G Novemba 28 dhidi ya Uswisi na Desemba 2 dhidi ya Cameroon baada ya kuumia kufundo cha mguu.
				
					



