Featured
Gwambina yaikamia Copco
KOCHA Mkuu wa Gwambina, Hassan Salum amesema timu yake imejipanga vyema
kwa mchezo wa ligi ya Championship dhidi ya Copco Veteran kwenye Uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza Oktoba 9.
Akizungumza na gazeti la HabariLEO, Salum amesema timu yake imejipanga kupata ushindi wake wa kwanza kwenye ligi hiyo.
“Mpaka sasa tumecheza michezo mitatu ya ligi ila bado hatujapata ushindi wowote lakini
tunaendelea kupambana kupata ushindi,” amesema Salum.
Amesema kuelekea mchezo huo hakuna majeruhi yoyote na wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri.
Amewaomba wadau na wapenzi wa soka wilayani Misungwi waendelee kuisaidia timu yao ifanye vema.




