EPL

Guardiola kumpumzisha Rodri

MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola anasema yuko tayari kumpumzisha Rodri baada ya kiungo huyo kusema anahitaji mapumziko.

Rodri, 27, amecheza mechi 41 msimu huu na alidokeza baada ya sare ya Jumanne ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid kwamba City walipanga kumpumzisha.

Kikosi cha Guardiola kitacheza na Luton uwanja wa Etihad leo.”Ikiwa mchezaji hataki kucheza basi hatacheza, rahisi,” alisema meneja wa Manchester City.

Katika ligi tano bora za Ulaya ni wachezaji watatu pekee ambao wameanza mara nyingi zaidi ya mchezaji wa kimataifa wa Uhispania msimu huu, beki wa Arsenal William Saliba ameanza 42.

“Angalia michezo yetu na kisha utagundua. Yeye ni muhimu sana kwa ubora anaoutoa,” aliongeza Guardiola, ambaye timu yake inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England zikiwa zimesalia mechi saba.

Related Articles

Back to top button