Africa

De Agosto wakataa mashabiki mechi ya Simba

DAR ES SALAAM: KLABU ya FC 15 de Agosto imekataa mashabiki kuingia uwanjani kwenye mchezo wao wa kwanza wataokuwa wenyeji mnamo Oktoba 20, mwaka huu.

Timu hiyo kutoka Guinea ya Ikweta imeridhia kukipiga Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama uwanja wao nyumbani lakini ikieleza haihitaji mashabiki uwanjani siku hiyo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ameeleza kuwa kwa muktadha huo mechi itakayohusisha mashabiki ni mechi yao ya marudiano katika uwanja huohuo ambapo Simba itakuwa nyumbani.

“Rasmi mechi zote mbili na de Agosto zitachezwa Uhuru lakini katika mazungumzo na de Agosto waligusia mechi yao ya nyumbani isiwe na mashabiki, hivyo mashabiki watakuwepo siku ya marejeano Simba ikiwa nyumbani,” alisema Ally.

Awali, de Agosto walitaka kupeleka mechi yao ya nyumbani ipigwe nchini DR Congo kutokana na changamoto ya uwanja waliyonayo.

Lakini baada ya majadiliano na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mechi hizo za raundi ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, zote zitapigwa Dar es Salaam.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button