Mastaa

D voice: Aeleza kwa nini hakumchangia matibabu mkubwa fella

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva kutoka lebo ya Wasafi, Abdul Khamis Mtambo maarufu kama D Voice, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ziara aliyofanya pamoja na Diamond Platnumz kwenda kumtembelea Mkubwa Fella wakati alipokuwa amelazwa hospitalini.

Akizungumza na waandishi wa habari, D Voice amesema kuwa licha ya kufika hospitalini mara moja au mbili akiwa na Diamond, hakuweza kuchangia gharama za matibabu kutokana na hali yake ya kifedha kwa kipindi hicho.

“Mimi binafsi nilikwenda kumuona mara moja au mbili nikiwa na Diamond Platnumz, lakini sikuwa na kitu cha kuchangia. Nilikuwa sina pesa kabisa, nilichoweza kufanya ni kumpa pole tu kwa wakati ule,” amesema D Voice.

Aidha, amesema kuwa hana taarifa juu ya kiasi cha fedha alichotoa Diamond kwa ajili ya matibabu ya Mkubwa Fella, akibainisha kuwa hakuhudhuria vikao vya michango kwa sababu hakuwa na uwezo wa kuchangia.

“Diamond alitoa shilingi ngapi sijui, kwa sababu sikuhudhuria vikao vya kumsaidia. Binafsi sikuwa na kitu cha kuchangia,” ameongeza.

Mbali na hilo, msanii huyo wa singeli ameweka wazi kuwa licha ya kipaji chake kikubwa cha muziki, anaamini pia ana uwezo mzuri katika fani nyingine.

“Mimi nje ya muziki, ni ‘ostadi’ mzuri tu,” amesema D Voice.

Related Articles

Back to top button