KwinginekoLa Liga

Barca hatihati kumpoteza Gavi bila malipo

TIMU za Liverpool na Manchester City zinajiweka tayari kwa ajili ya usajili baada kubainika kwamba mkataba wa Pablo Gavi katika klabu ya Barcelona una tatizo.

Gavi mwenye umri wa miaka 18 alisaini mkataba mwanzo wa msimu huu lakini mkataba huo umeripotiwa kuwa batili baada ya kurekodiwa isivyo sahihi Ligi Kuu Hispania, LaLiga.

Sasa Mahakama ya Catalan imeamua dhidi ya klabu hiyo ikiwa na maana Gavi ataondoka Camp Nou akiwa huru msimu huu.

Septemba 2022 alisaini mkataba mpya Barcelona wenye kipengele cha kuachiliwa chenye thamani ya pauni milioni 866.

Liverpool na Manchester City zinapenda uchezaji wa Gavi na zimetiwa moyo na hali hiyo ya hivi karibuni ya kimkataba ambayo inaweza kuziruhusu kumsajili.

Related Articles

Back to top button