Nyumbani
Babu Tale aituliza Simba

MBUNGE wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Shabani Taletale ‘Babu Tale’ ameipa moyo timu ya Simba kufuatia matokeo ya kusuasua hivi karibuni
Kauli hiyo ameitoa hii leo Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia katika mkutano 11 kikao cha 22 kuhusu bajeti ya Wizara ya Maji 2023/2024.
“Kwanza niipongeze timu yangu ya Simba kwa kuendelea kufa kiume, na watafufuka kiume.”
Itakumbukwa klabu ya Simba S.C imekuwa na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha hali inayowaondoa katika kugombania ubingwa wowote wa kimashindano msimu huu.