EPL

Arsenal ‘yamtwaa’ nahodha Brentford

LONDON, Washika mitutu wa jiji la London Arsenal wametangaza kumsajili aliyekuwa nahodha wa ‘The Bees’ Brentford FC Christian Norgaard katika hatua ya klabu hiyo ya London Kaskazini kuendelea kuimarisha safu ya kiungo kufuatia mwenendo mbaya mwishoni mwa kila msimu katika misimu ya hivi karibuni.

Taarifa za kifedha hazikufichuliwa lakini ripoti za vyombo vya habari vya England zinasema Arsenal imelipa ada ya awali ya pauni milioni 10 ambayo ni sawa na shilingi Bilioni 35.5 za kitanzania kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 31 kwa mkataba wa miaka miwili na chaguo la kuongeza mwaka wa tatu.

“Ni mchezaji wa kimataifa mwenye uzoefu mkubwa na ligi kuu. Amethibitisha ustadi wa uongozi na tabia thabiti ambayo itakuwa muhimu sana kwa kikosi chetu,”

“Ni kiungo mkabaji mwenye ufahamu bora wa kimbinu mwenye kucheza nafasi nyingi uwanjani. Pia ana umakini wa kimwili na akili ambayo itatupa upana na usawa wa kikosi. Christian ataleta mengi kwenye timu ndani na nje ya uwanja.” – kocha wa Arsenal Mikel Arteta amenukuliwa katika taarifa ya klabu hiyo

Norgaard anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa Arsenal mwishoni mwa msimu huu baada ya kuwasajili kipa Kepa Arrizabalaga kutoka Chelsea na kiungo mkabaji Martin Zubimendi kutoka Real Sociedad.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button