La Liga

Ancelotti: Tunajua kushinda bila Vini Jr

VALADOLLID: MENEJA wa mabingwa wa kihistoria wa ligi ya mabingwa barani Ulaya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema wanajua namna ya kushinda mechi zao bila ya kuwa na nyota wake Vinicius Junior ambaye ataukosa mchezo wa pili mfululizo wa Laliga.

Vinicius ambaye hakuwepo katika ushindi wa 4-1 kwa Las palmas wikiendi iliyopita hatakuwepo pia katika mchezo wa kesho dhidi ya Real Valladolid kwakuwa anatumikia adhabu ya kutocheza mechi mbili baada ya kupata kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Valencia Januari 3 mwaka huu na Ancelotti haoni pengo lake.

“Watu wanasahau tulishinda Mataji mawili ya ligi ya mabingwa bila Vini, ni mchezaji mzuri yuko hivyo muda wote lakini ni vyema pia akapata muda wa ‘kurecover’ ili awe mzuri zaidi katika kipindi hiki muhimu cha msimu” amesema

Real Madrid wana ratiba ngumu kwani wameshacheza mechi saba za mashindano yote hadi sasa tangu kuanza kwa Januari lakini wamefanikiwa kukalia kilele cha LaLiga wakiwa na pointi 46 katika mechi 20

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button