Al Hilal, Simba nani mbabe leo?

MENEJA wa Habari wa klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Al Hilal leo yanakwenda vizuri na wamejipanga kushinda kama ilivyokuwa mchezo wa kwanza dhidi ya Asante Kotoko.
Akizungumza na Spotileo, Meneja huyo amesema Kocha Mkuu Zoran Maki ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na timu yake na ameahidi kuzidi kufanya vizuri zaidi kwenye mechi zijazo.
“Kingine kocha amefurahi kupata mechi hizo sababu zimezidi kukiimarisha kikosi chake na kujenga muunganiko mzuri ambao ulikosekana kwenye mchezo mbili za Ligi Kuu,” amesema Ahmed.
Amesema dhamira ya Simba kushiriki michuano hiyo maalumu siyo kupata matokeo bali ni kupima ubora wa kikosi kabla ya kuanza mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika mwezi ujao.
Simba imepangwa kuanza hatua ya awali dhidi ya Nyasa Bullets ya Blantyre, Malawi Septemba 9.