Onana kuikimbia Arsenal, Kambwala Man United

LONDON, Uingereza: KIUNGO wa kati wa Everton, Amadou Onana, yuko mbioni kuikacha Arsenal kwa ajili ya kuhamia Aston Villa.
Onana ameichezea Everton mechi 72, zikiwemo 37 msimu uliopita katika mashindano yote baada ya kujiunga na Lille kwa pauni milioni 30 mwaka 2022.
Onana aliiwakilisha nchi yake kwenye Euro 2024, ambapo walitolewa na Ufaransa katika hatua ya 16 bora.
Katika hatua nyingine, Willy Kambwala anakaribia kusaini Villarreal.
Mtaalamu wa uhamisho wa soka, Fabrizio Romano, aliandika kwenye mtandao wake wa X kwamba: “Maelezo ya mkataba kati ya Villarreal na Man United kwa Willy Kambwala. Villa wanakaribia kukamilisha dili la pauni milioni 50 kwa Mbelgiji huyo, kwa mujibu wa Sky Sports.
Kocha Unai Emery anataka kuimarisha kikosi chake kabla ya kampeni yao ya Ligi ya Mabingwa kuanza.