Nyumbani

Breaking News: ‘Try Again’ aachia Bodi Simba SC

DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Klabu ya Simba Salum Abdallah ‘Try Again’ ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo. Ameweka wazi uamuzi huo leo alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Azam TV.

Katika maelezo yake Try Again amesema ameshauriana na Mwekezaji na rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’ na kuafikiana kwa pamoja kumpisha Mo katika kiti hicho.

Mhene amesema anatoka katika nafasi hiyo kupisha uimarishaji wa klabu hiyo ambayo kwa misimu takribani mitatu ya karibuni timu hiyo kuwa na mzoroto wa matokeo hali iliyoibua hali ya mchafukoge kwa takribani majuma mawili klabuni humo.

Related Articles

Back to top button