Kwingineko

West Ham yamtaka Goretzka kuwa mbadala wa Rice

WAGONGA Nyundo wa London, West Ham United imeripotiwa kutaka kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Leon Goretzka kama mbadala wa nahodha aliyeondoka Declan Rice.

Kwa mujibu wa mtandao wa michezo espn, Bayern ipo tayari kumuuza Goretzka mwenye umri wa miaka 28 majira haya ya joto huku kocha wa klabu hiyo Thomas Tuchel akitathmini namna ya kumpata namba 6 mpya.

Hata hivyo, licha ya uongozi wa Allianz Arena kutafuta ofa ya euro milioni 50 sawa na shilingi bilioni 130.4, Goretzka hadi sasa amekuwa akisisitiza nia yake ya kusalia klabuni hapo na amekataa ombi la kujadiliana vipengele binafsi.

Goretzka alikuwa na mchango mkubwa katika ubingwa wa Bayern wa Bundesliga msimu uliopita akifunga magoli matano katika michezo 27 ya ligi.

Kiungo huyo ana miaka mitatu imebaki katika mkataba wake wa sasa akiwa amesaini nyongeza ya miaka mitano 2021.

Related Articles

Back to top button