EPL

City kurudi kileleni leo?

BAADA ya Jana Ligi Kuu nchini England kupigwa mchezo mmoja, leo ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili, Man City itakuwa Etihad dhidi ya West Ham, Liverpool dhidi ya Fulham Uwanja wa Anfield.

Jana kulikuwa na mchezo mmoja ambapo Arsenal iliichapa Chelsea mabao 3-1 katika Uwanja wa Emirates.

Man City ina pointi 76 itaishusha Arsenal yenye pointi 78 kwenye nafasi ya kwanza mwa msimamo wa ligi endapo itashinda mchezo wao wa leo.

Kwa upande wa Liverpool wenye pointi 56 wanasaka nafasi ya kurudi kwenye nafasi nne za juu ili wapate nafasi ya kufuzu mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Michezo hiyo yote itapigwa saa 4:00 usiku.

Related Articles

Back to top button