Michezo MingineTennis
Nadal apoteza mchezo akirejea kutoka kupona majeraha

NYOTA wa tenisi Rafael Nadal ameshindwa na Borna Coric wa Croatia katika mashindano ya wazi ya Cincinnati ikiwa ni mchezo wa kwanza tangu alipojitoa nusu fainali ya Wembledon kwa sababu ya majeraha.
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 36 amepoteza 7-6(9-7) 4-6 6-3 kwa Coric ambaye anashika namba 152 kwa ubora duniani.
Nadal ametumia wiki sita kutibu majeraha ya misuli ya tumbo na kichapo hicho katika roundi 32 ya mchezo ni pigo kwa maandalizi yake kwa ajili ya mashindano ya wazi ya Marekani yaliyopangwa kuanza Agosti 28, 2022.
“Niliweza kucheza seti mbili tu kabla ya mchezo huu katika siku 40 zilizopita”, amesema Nadal ambaye alishinda mashindano ya wazi ya Marekani 2010, 2013, 2017 na 2019.