
MICHUANO ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) hatua ya 16 inaendelea leo kwa mechi tatu kupigwa Dar es Salaam, Geita na Singida.
Mabingwa watetezi Yanga itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons wenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Geita Gold itakipiga kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Nyankumbu dhidi ya Green Warriors wakati Singida Big Stars itaikaribisha JKT Tanzania kwenye uwanja wa CCM Liti, Singida.
Katika mchezo mmoja uliopigwa Machi 2 wekundu wa Msimbazi, Simba imeibugiza African Sports magoli 4-0 kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.