Featured

Newcastle kupata zaidi ya bil 2/- Carabao

WACHEZAJI wa klabu ya Newcastle United watagawana bonasi ya pauni milioni moja sawa na shilingi bilioni 2.79 iwapo watashinda fainali ya kombe la Carabao-(EFL) dhidi ya Manchester United Februari 26..

Iwapo Newcastle itatwaa taji hilo kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Wembley, London litakuwa kombe la kwanza katika muda wa miaka 48 iliyopita.

Bonasi hiyo ni mara kumi ya kiasi cha fedha za zawadi ambacho Newscastle itapata kutoka EFL kwa kushinda taji hilo lakini wamiliki wa klabu hiyo wanafurahi kuwapa zawadi wachezaji kwa kile kitakachoonekana kuwa mafanikio ya kihistoria.

Kwa mujibu wa zawadi za fedha za EFL, mshindi wa kombe la Carabao mwisho wa wiki hii atapata pauni 100,000 sawa na sh milioni 279 na mshindi wa pili pauni 50,000 sawa na sh milioni 139.5.

Related Articles

Back to top button