Filamu

Ramayana yavuna zaidi ya bilioni 13 kwa siku sita tu!

MUMBAI: FILAMU ya ‘Ramayana’, inayowashirikisha waigizaji nyota nchini India Ranbir Kapoor, Yash na Sai Pallavi, imeendelea kufanya vizuri katika soko la filamu, ikivutia watazamaji wengi tangu ilipoanza kuoneshwa.

Filamu hiyo imeonesha mafanikio makubwa katika mauzo ya tiketi, ambapo ndani ya siku sita pekee imekusanya zaidi ya rupia milioni 440, sawa na takribani bilioni 13.2 za Tanzania.
Mafanikio hayo yanaifanya ‘Ramayana’ kuwa miongoni mwa filamu zinazovutia hisia za mashabiki wa sinema, huku ikiendelea kuweka rekodi mpya katika soko la filamu.

Ranbir Kapoor, anayeigiza nafasi ya Bwana Rama, amekuwa miongoni mwa vivutio vikubwa vya filamu hiyo, huku Yash na Sai Pallavi nao wakichangia kuifanya kazi hiyo kuwa na mvuto wa kipekee.

Filamu hiyo imekuwa gumzo kutokana na ukubwa wa utayarishaji wake, mastaa wanaoigiza pamoja na simulizi inayotokana na hadithi maarufu ya Ramayana.

Hata hivyo, mwenendo wa mauzo ya tiketi katika siku zinazofuata utaamua iwapo itaendelea kuvunja rekodi zaidi na kujiimarisha kama mojawapo ya filamu zilizofanya vizuri zaidi katika soko la sinema.

Related Articles

Back to top button