Exim Benki yaunga mkono mbio za kitonga Kilolo

KILOLO, IRINGA — Benki ya Exim Tanzania imeunga mkono Mbio za Kitonga Marathon 2026 zilizofanyika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, katika jitihada za kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kuangazia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika wilaya hiyo.

Mbio hizo zilizofanyika chini ya kaulimbiu “Tunza Mazingira, Wekeza Kilolo” ziliwakutanisha washiriki na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika utunzaji wa mazingira, huku zikitoa fursa ya kuangazia uwezo wa Kilolo katika sekta za kilimo, utalii na biashara za wenyeji.
Benki ya Exim Tanzania, iliyokuwa Mdhamini Mkuu wa mbio hizo, ilisema ushiriki wake ni sehemu ya jitihada za kushirikiana na jamii na wadau katika masuala yanayochangia maendeleo endelevu.

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu, alisema udhamini huo unaakisi imani ya Benki kwamba jukumu la taasisi za kifedha haliishii katika kutoa huduma za kifedha pekee, bali pia ni kushiriki katika mipango inayolenga kuunganisha wadau katika kutekeleza vipaumbele vya maendeleo.
“Mbio za Kitonga zinatoa fursa ya kuitangaza zaidi Kilolo na uwezo wake wa kiuchumi, huku zikihamasisha uwajibikaji wa pamoja katika uhifadhi wa mazingira. Sisi Exim Bank tunaamini kuwa maendeleo endelevu yanahitaji ushirikiano kati ya jamii, wafanyabiashara na wadau wengine,” alisema Kafu.

Alisema udhamini huo unaendana na dhamira ya Benki ya kushirikiana na jamii inazozihudumia na kuunga mkono juhudi zinazolenga kuchangia maendeleo katika maeneo hayo.
Ushiriki wa Exim Bank katika mbio hizo ni sehemu ya mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii, Exim Cares, unaojumuisha shughuli mbalimbali katika maeneo ya afya, elimu, uhifadhi wa mazingira, ubunifu na elimu ya masuala ya fedha.

Mwaka 2026, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 29 tangu kuanzishwa kwake, Benki hiyo ilifanya shughuli za usafi katika jamii zinazozunguka matawi yake nchini.
Mkoani Iringa, timu ya tawi la Benki hiyo ilikabidhi vifaa vya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya FLERIMO kwa ajili ya kusaidia kuboresha usafi katika hospitali hiyo.

Exim Bank ilifungua tawi lake mkoani Iringa mwaka 2009, likitoa huduma za kifedha kwa watu binafsi, wafanyabiashara, kampuni na taasisi mbalimbali.

Kwa upande wa Kilolo, Mbio za Kitonga zimeweka pamoja ajenda ya uhifadhi wa mazingira na uhamasishaji wa fursa za kiuchumi, huku ushiriki wa wadau ukilenga kuongeza uelewa kuhusu nafasi ya jamii




