Sunderland yashinda dakika za mwisho

TORREENSE, URENO: TIMU ya Sunderland imepata ushindi wa kusisimua wa mabao 2-1 dhidi ya Torreense katika mchezo uliochezwa Ureno, baada ya Noah Sadiki kufunga bao la ushindi dakika ya 93.
Torreense, inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Ureno, iliwashangaza wageni wake kwa kupata bao la kwanza dakika ya 37 kupitia Volnei Feltes, aliyepiga shuti kali kutoka umbali wa takribani mita 27 na kumwacha kipa Robin Roefs bila nafasi ya kuokoa.
Kocha wa Sunderland, Régis Le Bris, aliwaingiza Granit Xhaka na Enzo Le Fée kabla ya dakika ya 60, mabadiliko yaliyochangia kuimarika kwa timu hiyo. Jules Ahoka alisawazisha kabla Sadiki hajafunga bao la ushindi katika dakika za mwisho.
Sunderland ilinyimwa penalti ya dakika za mwisho baada ya mapitio ya VAR, lakini hatimaye iliondoka na pointi zote tatu.
Kocha wa Torreense, Carlos Simões, alisema kufungwa bao katika dakika za mwisho kulikuwa pigo kubwa kwa wachezaji wake, ambao walibaki wamevunjika moyo baada ya kukaribia kupata sare.




