Kwingineko

McTominay atupia bao la kideo Scotland ikifuzu WC2026

GLASGOW: KIUNGO wa wababe wa Serie A SSC Napoli Scott McTominay alifunga bao maridadi kwa “bicycle kick” dakika tatu baada ya kuanza kwa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia (WC2026) wa Scotland dhidi ya Denmark usiku ya Jumanne.

Ben Gannon-Doak aliutuma mpira wa krosi ya juu kutoka upande wa kulia na McTominay akaufuata akiwa amegeukia upande tofauti na lango. Alipiga shuti safi la scissor-kick kutoka karibu na eneo la penalti.

Nyota wa tenisi wa Scotland Andy Murray kupitia ukurasa wake wa mtandao X alionesha kufurahishwa na goli hilo huku akionesha kutoamini namna Nyota huyo wa zamani wa Manchester United alivyofunga.

Scotland imefuzu kwa michuano hiyo ya mwakani inayoandaliwa kwa Pamoja na Marekani, Canada na Mexico baada ya kuifunga Denmark mabao 4-2 na kuongoza Kundi C kwa pointi 13 huku Denmark wakishika nafasi ya pili kwa pointi 11

Related Articles

Back to top button