EPL

Chelsea yakwaa kesi 74

LONDON: MABINGWA wa Dunia Chelsea ‘The Blues’ wamefunguliwa mastaka 74 na Chama cha Soka cha England (FA) kwa madai ya kukiuka kanuni zinazohusiana na malipo kwa mawakala kati ya mwaka 2009 na 2022. Mashtaka hayo kimsingi yanalenga matukio yaliyotokea kati ya msimu wa 2010/11 hadi 2015/16.

Kanuni zinazodaiwa kukiukwa na mabingwa hao wa zamani wa England zinahusu mawakala, madalali wa biashara (intermediaries) na uwekezaji kwenye biashara ya wachezaji.

Ikiwa watakutwa na hatia katika mshataka hayo Chelsea, wanaweza kukumbana na faini kubwa, kufungiwa kusajili na kukatwa pointi. Lakini wanaweza kulegezewa Kamba kidogo ikiwa watatoa ‘ushirikiano wa hali ya juu’ kwa wachunguzi wa Sakata hilo.

Katika kipindi ambacho Chelsea walitajwa kukiuka kanuni hizo klabu ilikuwa chini ya Bilionea wa Urusi Roman Abramovich aliyeanza kuimiliki kuanzia mwaka 2003 hadi 2022. Aliiuza Chelsea kwa muungano wa wafanyabiashara wanaoongozwa mwekezaji Mmarekani Todd Boehly na kampuni binafsi ya Clearlake Capital.

Baada ya Chapisho la FA muda mfupi Chelsea ilijibu kwa kutoa taarifa ya klabu, ambayo ilifichua kuwa “walijiripoti” kwa FA juu ya madai hayo. The Blues pia walionesha “shukrani” zao kwa FA na wanatumai suala hilo litahitimishwa “haraka iwezekanavyo”.

“Mara baada ya kukamilika kwa ununuzi, klabu iliripoti masuala haya kwa wadhibiti wote wanaohusika, ikiwa ni pamoja na FA. Klabu imeonesha uwazi usio na kifani wakati wa mchakato huu, ikiwa ni pamoja na kutoa ruhusa ya kufunguliwa na kusomwa kwa mafaili ya klabu na data zake.” – ilisema sehemu ya taarifa ya Chelsea

Julai 2023, Chelsea ilitozwa faini ya Pauni milioni 8.6 na UEFA kwa kuvunja sheria za ‘Financial Fair Play’ kutokana na “kuwasilisha taarifa zisizo kamili za kifedha” kati ya 2012 na 2019. Ukiukaji huo uliripotiwa na mmiliki mpya wa Stamford Bridge baada ya kuuzwa kwa klabu hiyo mwezi Mei mwaka 2022.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button