EPL

Kai Haverts hatihati kumaliza msimu

LONDON: WASHIKA mitutu wa Jiji la London Klabu ya Arsenal wamepata pigo kubwa baada ya mshambuliaji wao Kai Havertz, kupata jeraha la goti jambo linalotia shaka juu ya kupatikana kwake msimu huu ukiwa ndio kwanza umeanza na ukitazamiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

jarida la The Athletic limeripoti kuwa Mshambuliaji huyo raia wa Ujerumani wa mbioni kuanza kuuguza jeraha lake hilo na yupo katika hatua ya awali hivyo bado haitambuliki atakaa nje kwa muda gani.

Inaelezwa kuwa taarifa hiyo inaweza kuwafanya Arsenal kurudi sokoni kutafuta mshambuliaji mpya wa kusaidiana na Viktor Gyokers kabla ya dirisha la usajili kufungwa, kwani mshambuliaji mwingine Gabriel Jesus bado anaendelea na matibabu baada ya kupata jeraha la ACL msimu uliopita.

Hii ni mara ya pili kwa Havertz kupata jeraha linalomuweka nje kwa muda mrefu baada ya kufanyiwa upasuaji wa nyama za paja mwezi Januari.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button