Muziki

Director P aibuka upya na “Met You”,

Ree aonja ladha ya Afrika

CANADA:MSANII wa kizazi kipya na mwandaaji wa filamu mwenye asili ya Zambia na Kongo anayeishi nchini Canada, Patrick Lupasa ‘Director P’, ameibuka upya na ngoma yake mpya Met You ambayo imepenya kwa kasi kubwa miongoni mwa mashabiki barani Afrika, kinyume na matarajio yake ya awali.

Akizungumza na SpotiLeo, Director P amesema wimbo huo, amemshirikisha mwimbaji Ree mwenye asili ya Jamaica na Canada, ulitoka hivi karibuni na alidhani ungepata umaarufu zaidi ughaibuni. Hata hivyo, mashabiki wa Afrika wameupokea kwa shangwe kubwa.

“Nilitarajia Met You itabamba zaidi nje ya bara, lakini nimevutwa na jinsi mashabiki wa Afrika walivyoipokea. Ni wimbo wa mapenzi, na sasa niko kwenye maandalizi ya video ili kuendeleza burudani,” amesema Director P.

Ameeleza kuwa Met You ni hadithi ya mapenzi inayounganisha tamaduni kupitia lugha na ladha za muziki.

“Wimbo huu unagusa namna upendo unavyosikika unapozungumzwa kwa lugha nyingi. Ree ameleta ladha ya Karibea, nami nimechangia utamu wa Afrika Mashariki. Ni zaidi ya hadithi ya mapenzi, ni muunganisho wa kitamaduni,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button