Kwingineko

Dortmund yaitia kiwewe Mamelodi Sundowns

CINCINNATI, Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini inatumai hali ya hewa ya jiji la Cincinnati itawapa nafasi ya kufaulu dhidi ya wababe wa Bundesliga Borussia Dortmund wawili hao watakapokutana kwenye mchezo wa kukata na shoka wa Kombe la Dunia la Klabu saa moja usiku wa leo Jumamosi.

Sundowns, ambao walikuwa washindi wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika mapema mwezi huu, wapo kileleni mwa Kundi F baada ya kuifunga Ulsan HD ya Korea Kusini bao 1-0 katika mchezo wao wa ufunguzi lakini wanatazamiwa kuwa timu ya pili dhidi ya Dortmund kwenye Uwanja wa TQL.

Kocha wa klabu hiyo Miguel Cardoso, hata hivyo, ametahadharisha kuwa matokeo ya kutatanisha yanawezekana hata kama uwezekano wa hilo kutokea kuwa mdogo sana.

“Lolote linaweza kutokea wakati imani ya kiakili ya timu inapokuwa na nguvu na uhusiano wao wa kisaikolojia ni mkubwa kama ninavyoona hivi sasa ni wazi maajabu yanaweza kutokea” Cardoso aliuambia mkutano wa wanahabari.

“Na hicho ndicho nitajaribu kutengeneza kama mazingira rafiki kwenye timu uchu, imani, uamuzi na hisia sahihi ya kucheza mchezo kama huo na kutoa matokeo mazuri.” aliongeza

Kocha Cardoso aliweka wazi kuwa anatarajia kwamba timu yake, ambayo kwa kawaida hufurahia umiliki wa mpira haitaona hilo likitokea huku akiingia na hofu kwa safu yake ya ulinzi na ukali wa Dortmund ambao kwa mujibu wake wamefunga mabao asilimia 40 kwa ‘counterattack’

Related Articles

Back to top button