Kwingineko

Bayern yajitwisha heshima ya bara Ulaya

MIAMI, Mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich imetoa somo la namna ya kutetea heshima ya bara la Ulaya kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Klabu, ikipambana katika mechi yenye upinzani mkali na kuibuka na ushindi mgumu wa 2-1 dhidi ya Boca Juniors na kutinga hatua ya 16 bora.

Wakiungwa mkono na kishindo cha mashabiki waliovalia bluu na njano waliougeuza Uwanja wa Hard Rock kuwa kituo hatari chenye kelele cha “Bombonera”, Boca Juniors walipambana vikali, lakini Bayern walionesha ukubwa wao katika dakika za mwisho.

Baada ya Harry Kane kuwapa mabingwa hao wa Ujerumani bao la mapema, Boca walisawazisha kupitia kwa Miguel Merentiel, Kabla ya Michael Olise kupachika bao la ushindi dakika za lala salama lililoipandisha Bayern kileleni mwa Kundi C kwa pointi sita, mbili mbele ya Benfica.

Boca, na pointi yao moja, wanasalia kwenye mshike mshike wa kusaka nafasi yao kwenye hatua ya 16 bora huku watakapomenyana na mastaa Auckland City katika raundi ya mwisho ya mechi huku Bayern wakichuana na Benfica.

Ushindi huo wa Bayern Munich unazifanya timu za Ulaya kupata mwanga wa kurejea tena baada ya kukabiliwa na kibarua kigumu kabiliwa kwenye michuano hiyo mwaka huu huku klabu kama FC Porto, Paris St Germain na Chelsea zikipata vipigo katika mechi zao za karibuni .

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button