Tom Cruise: Soko la filamu za Marekani limeshuka mno nchini China

BEIJING: MCHEZA filamu Tom Cruise amesema kutokuaminiana kati ya Washington na Beijing kwa siku za karibuni kumeporomosha mauzo ya filamu za Hollywood nchini China.
Tom Cruise takwimu zinaonesha kwamba mvutano unaoendelea wa kisiasa kati ya China na Marekani ndiyo chanzo kikubwa kinachoongeza ugumu wa kupata watazamaji wa filamu zao kwa watu wa China tofauti na ilivyokuwa zamani.
Aprili mwaka huu, Beijing ilisema itapunguza idadi ya filamu za Marekani zinazoruhusiwa sokoni kama sehemu ya mwitikio mpana wa msuguano wa kibiashara kati ya Washington na Beijing na mazungumzo ya awali kumaliza mvutano huo yamekwama.
Lakini licha ya changamoto hizo filamu ya Mission: Impossible – The Final Reckoning ya Tom Cruise, imeongoza kwa mauzo na idadi kubwa ya watazamaji nchini China katika ufunguzi wa filamu hiyo hivi karibuni.
Katika uoneshaji huo wa awali. Dola milioni 25.2 zilipatikana katika maeneo 11,847 nchini China wakati wa ufunguzi.
Filamu hiyo pia imefanya vizuri zaidi nchini Marekani kwa mwaka huu wa 2025, ikiipita Filamu ya Warner Bros Entertainment Inc. ya A Minecraft ambayo ilikusanya dola milioni 29 tangu ilipoanza kuoneshwa Aprili 4.
The Mission Impossible Franchise imeleta matumaini kwa filamu za Kimarekani nchini China, kama ilivyokuwa hapo awali ambapo mwaka 2018 filamu hizo zilifikia kilele cha soko ambapo karibu dola milioni 77 zilikusanywa nchini China.
Lakini kwa sasa zimeshindwa kupata umaarufu nchini China. Minecraft ilifunguliwa na dola milioni 14.5, wakati Thunderbolts na Lilo & Stitch ya Walt Disney Co. ilileta dola milioni 10.5 na dola milioni 8.7, mwishoni mwa wiki.