Filamu

Muigizaji akataliwa kuigiza filamu kisa mwembamba

INDIA:MWANAMUZIKI Surveen Chawla ameshangaza mashabiki na wadau wa filamu baada ya kudai kwamba alitakiwa awe na uzito mkubwa ndipo apewe nafasi ya kucheza katika filamu za kusini India.

“Niliambiwa mimi ni mwembamba sana na sina matiti makubwa hivyo siwezi kuigiza katika filamu za Kusini mwa India.’ Surveen Chawla ameeleza akidai kwamba jambo hilo limemshangaza licha ya kuigiza filamu nyingi za India hakuwahi kukutana na changamoto kama hiyo.

Muigizaji Surveen Chawla alianza safari yake ya uigizaji na vipindi vya televisheni kama vile ‘Kahin To Hoga na Kaajjal’, na baadaye akatambulika kwa uigizaji wake katika sinema ya Kipunjabi na Kihindi.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na Hauterrfly, Surveen amesema ameshangazwa alipoombwa aongeze uzito ili kufanya kazi katika sinema ya Kusini. “Ubaguzi wa kijinsia katika tasnia ya filamu upo kila mahali, niliombwa niongeze uzito ili kufanya kazi katika sinema ya Kusini na pia walisema sina matiti makubwa,” Surveen Chawla.

Alipoulizwa kama kweli waigizaji wanahitaji kunenepa kufanya kazi katika sinema ya Kusini, Surveen alisema, “Ndiyo, niliambiwa kuwa wewe ni mwembamba sana, mwembamba kwa sababu hauna matiti makubwa,”.

Surveen amecheza filamu nyingi ikiwemo ‘Hum Tum Shabana’ ya mwaka 2011, ‘Taur Mittran Di, Saadi’ Love Story, ‘Singh vs Kaur’, ‘Parch Story’ na nyingine nyingi kwa sasa anaonekana katika kipindi cha Jinai 4. Kipindi hiki pia kinaigizwa na Pankaj Tripathi, Asha Negi, Shweta Basu Prasad, Mita Vashisht, na Zeeshan Ayyub.

Related Articles

Back to top button