Kwingineko

Inter Milan kuvaa dhahabu kwenye fainali ya UCL

MILAN: WANAFAINALI wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Inter Milan watavaa jezi yao ya tatu (third kit) yenye rangi ya njano dhahabu watakapokutana na Paris St Germain jijini Munich katika mchezo wa kukata na shoka wa fainali ya Ligi hiyo ikiwa ni mechi ya kwanza rasmi kukutanisha miamba hiyo ya soka kutoka Italy na Ufaransa

Inter wameshacheza fainali sita za Ligi ya mabingwa (Kombe la Ulaya zamani) mpaka sasa huku ya kwanza ikiwa mwaka 1964 lakini hawajawahi kutumia jezi yao ya tatu katika mechi muhimu kama hii hadi sasa huku PSG watakaokuwa kama timu ya nyumbani wakitarajiwa kuvaa jezi yao ya nyumbani yenye rangi kuu ya bluu.

Waitaliano hao hata hivyo hawakuchagua kuvaa jezi yao ya pili yani jezi ya ugenini huku vijana hao wa Simone Inzaghi wakihusishwa na Imani za kishirikina kwakuwa wameshinda mechi zote za UCL wakiwa na jezi hiyo na kumbukumbu ya hivi karibuni zaidi ni ushindi wa 2-0 dhidi ya Feyenoord kwenye hatua ya 16 bora mwezi machi.

Kipigo pekee walichopata kwenye ligi ya Mabingwa msimu huu kilitoka kwa vijana wa kocha mpya wa Real Madrid Xabi Alonso Bayer Leverkusen na Inter Milan walivaa jezi zao nyeupe za ugenini. Katika fainali hiyo itakayopigwa Jumamosi watavaa jezi wanazoamini zina Bahati nao. Swali ni je watatoboa?

Related Articles

Back to top button