Mastaa

Mei 28 Tanzania, Nigeria macho yote kutua Tanzania

DAR ES SALAAM:MSANII nguli wa muziki wa Bongo Fleva, Juma Mkambala maarufu kama Jux, ametangaza rasmi tarehe ya sherehe ya saba ya ndoa yake, itakayofanyika nchini Tanzania katika ukumbi wa kifahari wa The Super Dome uliopo Masaki, jijini Dar es Salaam.

Baada ya kufanya sherehe sita za kifalme nchini Nigeria, Jux sasa anarudisha furaha hiyo nyumbani kwa kilele cha maadhimisho ya ndoa yake na mrembo Prisila.

Hafla hiyo ya kipekee inatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano, Mei 28, na tayari wageni maarufu kutoka Nigeria na mataifa mengine wameshaanza kuwasili kwa ajili ya maandalizi.

Masaki inatarajiwa kusimama kwa muda huku macho ya mashabiki na wapenzi wa muziki yakielekezwa kwa wawili hao wanaofunga rasmi pingu za maisha kwa mbwembwe.

Swali kubwa linalozungumzwa mitandaoni ni: Je, MC wa tukio hilo atakuwa nani? Na ni msanii gani hapaswi kabisa kukosa kupanda jukwaani usiku huo wa kihistoria?

Muda ukizidi kuyoyoma kuelekea Mei 28, sherehe hii inatarajiwa kuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya kijamii na burudani nchini kwa mwaka huu.

Related Articles

Back to top button