Mastaa

Kesi ya Sean “Diddy” Combs Imeahirishwa

MAREKANI:MAHAKAMA inayosikiliza kesi ya Sean “Diddy” Combs ya ulaghai na ulanguzi wa ngono imetupilia mbali kesi hiyo kwa siku moja baada ya kupokea ushahidi kutoka kwa mashahidi watatu.

Katika mwendelezo wa kesi hiyo, mashahidi muhimu walitoa ushahidi siku ya Jumatatu kuthibitisha madai ya unyanyasaji dhidi ya Cassie Ventura. Dawn Richard, mwanamuziki wa zamani wa kundi la Danity Kane, alieleza jinsi alivyoshuhudia Combs akimpiga Cassie.

Kerry Morgan, rafiki wa karibu wa Cassie, alisimulia juhudi zake za kumshawishi aachane na uhusiano huo wa mateso.

Naye David James, msaidizi wa zamani wa Combs, alielezea mazingira ya hofu aliyokuwa akifanya kazi ndani yake, akisema: “Hii ni himaya ya Bwana Combs.”

Mawakili wa Combs walijitahidi kuonesha mashahidi hao kama watu wasioaminika. Ingawa Combs amekana mashtaka ya ulanguzi wa ngono na kuendesha mtandao wa kihalifu, amekiri kuwa na historia ya matumizi ya dawa za kulevya pamoja na unyanyasaji wa nyumbani.

Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea Jumanne, ambapo ushahidi wa kina zaidi unatarajiwa kutolewa, ukiwemo kutoka kwa mtu anayefahamika kwa jina la “The Punisher” na mama wa Cassie.

Related Articles

Back to top button