La Liga

Yamal hang’oki Barca

BARCELONA: Kinda wa FC Barcelona Lamine Yamal ameweka wazi kuwa ana mpango wa kusaini mkataba wa kuendelea kusalia katika kikosi cha vinara hao wa Laliga kwa kuwa ana mapenzi makubwa na klabu hiyo.

Yamal amekiambia chombo cha habari cha Mundo Deportivo cha Hispania kuwa anaipenda sana Barcelona na kwa sasa angependa kusalia na klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi ili awe sehemu ya mafanikio yajayo ya klabu hiyo kwa kuwa bado ana deni nayo.

“Barcelona inanidai bado, kila kitu kipo sawa hapa nina furaha, nimepokelewa vizuri na uongozi na wachezaji wenzangu wamenionesha upendo mkubwa sana tangu nimefika hapa”

“Hakuna asiyejua ukubwa wa ushabiki wangu kwa Barcelona na ni kiasi gani nataka kubaki hapa kwa hiyo, ndio nitaongeza mkataba” amesema Yamal

Aidha winga huyo amekanusha tetesi za hapo awali zilizomhusisha na mabingwa wa Ligue 1 PSG akisema kuwa hajapokea ofa yeyote kutoka Paris akiongeza kuwa ana mkataba na ingekuwa ngumu kwake kuihama Barcelona.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button