Muziki

Sauti za Busara 2025 kufanyika siku ya wapendanao

ZANZIBAR: TAMASHA la 22 la Kimataifa la Muziki la Sauti za Busara kwa mwaka 2025 linatarajiwa kufanyika Februari 14 hadi 16 katika Mji Mkongwe, Zanzibar.

Tamasha hilo maalumu kwa muziki wa kiafrika linafanyika kwa muziki wa kiafrika na urithi wa kitamaduni utakaopigwa ‘Live’ na wanamuziki kutoka mataifa mbalimbali duniani kote.

Msanii kutoka Afrika Kusini, Thandiswa Mazwai ndiye Msanii Mkuu wa Tamasha hilo.
Thandiswa, aliyejizolea umaarufu mkubwa katika kipindi cha baada ya utawala wa ubaguzi wa rangi (Apartheid), ameendelea kuwa alama ya muziki katika kupigania haki na mabadiliko.

Anatumia muziki wake sio tu kama njia ya kujieleza, bali pia kama njia ya kusherehekea uhuru na furaha!

Thandiswa Mazwai si msanii anayetumia sauti yake na akitumia muziki wake kushiriki mazungumzo ya kijamii na kuhamasisha watu kusherehekea na kudumisha urithi wa kitamaduni wa Afrika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button