Kwingineko

Afrika Kusini kuanza kutumia VAR Aprili

WAZIRI wa michezo wa Afrika Kusini Gayton McKenzie amesema kuwa teknolojia ya usaidizi wa muamuzi kwa njia ya video VAR itaanza kutumika katika ligi kuu ya nchini humo PSL kufikia mwishoni mwa April kabla ya msimu huu kumalizika.

McKenzie ambaye mwaka uliopita aliapa kupambana kwa uwezo wake wote kuhakikisha anazima vilio vya mashabiki juu ya maamuzi tata ya waamuzi kwenye ligi hiyo ambayo alidai kwa kiasi kikubwa yanatokana na waamuzi kuchukua rushwa.

“Niliwaahidi raia wa Afrika kusini kuwa VAR inakuja, nilisema mwisho wa mwezi Aprili na hakuna kilichobadilika, najua kuna timu zinahofia ujio huu kwa sababu ni wanufaika wakubwa wa maamuzi mabovu sitaki kuwataja mnawajua lakini wanaopenda mpira wa haki bila shaka wanafurahia ujio huu nadhani sasa muda umefika wa kukomesha rushwa kwa waamuzi” McKenzie aliiambia SABC

Ligi kuu ya Afrika Kusini kama ligi nyingine barani Afrika zimekuwa zikizongwa na lawama za mashabiki juu ya maamuzi tata ya waamuzi lakini sasa huenda ikawa ya kwanza barani humu kutumia teknolojia hiyo ambayo Tanzania pia iko njiani kuianza.

Related Articles

Back to top button