Mastaa

Gigy Money apoteza akaunti yake ya Instagram

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’, ameripotiwa kupoteza tena akaunti yake ya Instagram iliyokuwa na takribani wafuasi milioni tano.

Hii ni mara ya pili kwa msanii huyo kupoteza akaunti ya Instagram yenye idadi kubwa ya wafuasi, baada ya awali kupoteza akaunti iliyokuwa na karibu wafuasi milioni nne.

Kwa sasa, Gigy Money anapatikana Instagram kupitia akaunti ya Gigy Money For Now, ambayo awali ilikuwa ikitumika kuchapisha maudhui yanayomhusu binti yake, Mayra.

Hata hivyo, sababu za kupotea kwa akaunti hiyo mpya yenye mamilioni ya wafuasi bado hazijafahamika, huku ikisubiriwa taarifa zaidi iwapo iliondolewa na Instagram, ilivamiwa au imekumbwa na changamoto nyingine za kiufundi.

Kupotea kwa akaunti hiyo kunaweza kuathiri mawasiliano ya msanii huyo na mashabiki wake pamoja na shughuli zake za kutangaza muziki na kazi nyingine kupitia mtandao huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button