Africa

Yanga kumaliza leo?

WAWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga leo inashuka dimbani dhidi ya ASAS Djibouti ukiwa mchezo wa marudiano kuamua timu ipi itasonga mbele kwenye michuano hiyo.

Mchezo huo ambao Yanga imeupa kauli mbiu ‘๐Œ๐€๐— ๐ƒ๐€๐˜, Wananchi ๐๐ข ๐Œ๐ฐ๐ž๐ง๐๐จ ๐–๐š ๐Š๐ฎ๐œ๐ก๐จ๐ฆ๐ž๐ค๐ž๐š ๐“๐ฎ!’ utafanyika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Agosti 20 Yanga ilishinda kwa mabao 2-0, ASAS Djibouti ikiwa mwenyeji kwenye uwanja huo huo.

Mshindi wa jumla atakutana na Al-Merreikh ya Sudan iliyoitoa AS Otoho ya Jamhuri ya Congo katika hatua inayofuata.

Related Articles

Back to top button