EPL

Walker akoshwa na Reece James

MANCHESTER Nyota wa mabingwa mara nne mfululizo wa ligi kuu ya England Manchester City, Kyle Walker amemmwagia sifa nahodha wa Chelsea, Reece James kama beki bora wa kulia duniani.

Alipoulizwa kutaja beki bora zaidi wa kulia duniani kwenye ‘podcast’ ya You’ll Never Beat Kyle Walker “ beki huyo matata wa kulia alisema Reece James Ana kila kitu anachohitaji kuwa beki bora.

“Nadhani kama ningepata nafasi ya kuunda beki bora wa kulia angekuwa yeye (Reece), ana nguvu zangu, kasi ya Hakimi, uwezo wa kiufundi wa Cancelo, pasi za Trent [Alexander-Arnold], akili ya Carvajal na nadhani Reece anaujua zaidi mpira kwakuwa amecheza kama kiungo kwa muda mrefu”. Alisema Walker.

“Lakini kama ningewakusanya wote, na nichague ningemchagua Reece. Anakupa kila kitu.” aliongeza

Reece James amekosa sehemu kubwa ya msimu wake wa kwanza kama nahodha wa Blues kutokana na tatizo la misuli ya paja na ‘career’ yake kwa ujumla imeandamwa na jinamizi la majeraha.

Related Articles

Back to top button