Nyumbani

Ukubwa wa Yanga ni maono ya viongozi- Chicharito

WAKATI wengi wakidhani ukubwa na ubora wa Yanga unatokana tu na wachezaji wazuri, imetajwa pia maono ya viongozi wao ndiyo sababu kubwa ya timu hiyo kupiga hatua.

Akizungumza na HabariLEO, mtunza vifaa wa timu hiyo, Godlisten Anderson ‘Chicharito’ amesema licha ya kufanya vizuri kwa timu hiyo ila mashabiki pia wamekuwa sehemu ya mafaniko ya timu hiyo.

“Mtu akipenda Yanga anapenda kweli, huu ni mfano ambao tunauomba miaka yote, timu iwe bora isiwe bora mashabiki hawajawahi kukata tamaa,” amesema Chicharito.

“Pia ukubwa wa Yanga umetokana na umri, lakini makombe, ubora wa wachezaji timu za taifa, pia mashabiki wengi ndani na nje ya nchi,” ameongeza Chicharito.

Amesema mashabiki wa timu hiyo wamekuwa bega kwa bega na timu yao na hawajawahi kukata tamaa.

Related Articles

Back to top button