Africa
Twiga Stars kupindua meza leo?
TIMU ya taifa ya soka ya wanawake (Twiga Stars) leo ina kibarua cha kupindua meza katika mchezo wa marudiano kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Africa kwa wanawake (WAFCON 2024).
Mchezo huo utafanyika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Yamoussoukro, Ivory Coast Septemba 22, Twiga Stars ilikubali kipigo cha mabao 2-0.
Fainali za WAFCON 2024 zimepangwa kufanyika Morocco.