Tetesi

Tetesi za Usajili

BARCELONA imefanya mawasiliano na wawakilishi wa winga wa Athletic Club, Nico Williams kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo kuhamia Catalonia majira yajayo ya kiangazi. Mwaka huu Aston Villa imejaribu lakini imeshindwa kufikia dili na mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania.(SPORT)

Mbali na Williams, Barcelona pia inamtupia jicho beki wa kati wa Girona, Arnau Martinez ili kumsajili mwaka ujao.(Fichajes)

Real Madrid itaangalia uwezekano wa kumsajili nahodha wa Chelsea, Reece James ama mwaka 2024 au 2025 wakati ikiendelea na juhudi za kumsajili mrithi wa muda mrefu wa beki wa kulia wa sasa Dani Carvajal.(AS)

Wachezaji wa Arsenal Martin Odegaard na Ben White wanatarajiwa kusaini mikataba mipya ya muda mrefu Emirates.(Daily Mail)

Manchester United inaendelea kufuatilia maendeleo ya mshambuliaji Evan Ferguson, ambaye anaweza kuondoka Brighton & Hove Albion mwaka ujao.(Daily Mail)

Manchester City imefikia makubaliano kimsingi kumsajili kinda wa Argentina, Valentin Barco mwenye umri wa miaka 19 kutoka Boca Juniors.(TyC Sports)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button