Nyumbani

Stars kukipiga kirafiki dhidi ya Sudan

WACHEZAJI 21 wa kikosi cha timu ya taifa ya mpira wa miguu(Taifa Stars) wanaondoka Mei 8 kuelekea Saudi Arabia kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Sudan.

Kikosi hicho kitakachokuwa chini ya Kocha Hemed Suleiman ni magolikipa Ahmed Suleiman, Ally Salim na Abrahman Nassoro,

Mabeki ni Mukrim Abdallah, Alphonce Msanga, Miano Danilo, Gadiel Michael, Abdulmalik Zakaria, Baraka Mtuwi na Abdulrahim Bausi.

Viungo waliochaguliwa ni Mohamed Sagaf, Morice Abraham, Khalid Idd, Ishaka Mwinyi na Jabir Mpanda.

Washambuliaji wa kikosi hicho ni Omary Omary, Ben Starkie, Oscar Paul, Kelvin John, Tarryn Allarakhia na Ibrahim Ahmada.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button